Msingi wa imani yetu

Tumejikita katika kueneza Injili “kamili” inayomhudumia mwanadamu kupitia huduma za kiroho, kijamii, kiuchumi na kimazingira ili kuwa na jamii ya kikristo inayompenda Mungu na hivyo kutimiza utume wa Mungu katika maisha yetu.

“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi ...”
Mathayo 28:19

MAONO

Kuufanya Ulimwengu unaoshuhudia Neema ya Mungu na Upendo wa Kristo unaotolewa kwa watu wote.

DHAMIRA

Pamoja katika Kristo tunawekwa Huru kwa Neema ili tuishi kwa Uaminifu, Ushuhuda kamili na kutumika kwa furaha.

MIIKO YA USHARIKA CHINI YA DAYOSISI

  1. Msamaha na upatanisho.
  2. Utu, uhuru na haki.
  3. Umoja katika kutofautiana.
  4. Ujasiri na uwazi katika kuleta mabadiliko.
  5. Uaminifu na uwakili katika uumbaji wa Mungu.

VIPAUMBELE VYA USHARIKA CHINI YA MPANGO MKAKATI WA DAYOSISI

  1. Kuhakikisha ukuaji endelevu wa Kanisa na Dayosisi.
  2. Kutafuta fedha ili kukuza uchumi wa Kanisa na Dayosisi.
  3. Kuleta uongozi bora wa Kanisa na Utendaji fanisi.
  4. Kutoa huduma bora za kijamii.
  5. Kuhakikisha utunzaji bora wa Mazingira, Jamii, Uchumi na Siasa.

Huduma utakazopata ukitembelea Usharika wa Ebenezer:

  • Mafundisho ya Neno la Mungu
  • Maombi na Maombezi
  • Vipindi vizuri vya Kumsifu na Kumuabudu Mungu
  • Huduma ya Sakramenti takatifu
  • Huduma za ubatizo
  • Huduma mafundisho ya ndoa na Kufunga ndoa
  • Huduma mbali mbali za Kidiakonia
  • Shughuli mbalimbali za Vijana, watoto, Wakina mama na wakina baba
  • Ibada za nyumba kwa nyumba
  • Uimbaji kupitia vikundi mbalimbali (kwaya)