Jengo la kanisa la Ebenezer

Nyumba yetu ya ibada — karibu

Askofu Dk. Christian Ndossa

Askofu Dk. Christian Ndossa

Mkuu wa K.K.K.T. Dayosisi ya Dodoma

Mch. Grace Mbata

Mch. Grace Mbata

Mchungaji Kiongozi K.K.K.T. Usharika wa Ebenezer

Karibu

K.K.K.T Ebenezer — Imani, Tumaini, na Upendo

Tunaamini katika utatu mtakatifu wa Mungu; Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tumejengwa ndani ya msingi wa Yesu Kristo mwenyewe — msingi ulio wa pekee na usiokosea kwa mafundisho na maisha ya kanisa, kama ilivyo katika Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Agano Jipya.

Pia tunaamini katika Imani ya Mitume, Nikea, Athanasio na maungamo ya kanisa la Kilutheri, hasa katika Ungamo lisilobadilishwa la Augsburg na Katekisimo Ndogo ya Dk. Martin Luther.

Tunakukaribisha ushiriki pamoja nasi katika ibada — karibu.

Ebenezer

“… Hata sasa BWANA ametusaidia.”

1 Samueli 7:12b (SUV)

Usharika wa Ebenezer ni miongoni mwa sharika 53 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Dodoma.

Vilevile, Usharika huu ni miongoni mwa sharika 27 za Jimbo la makao makuu ndani ya Dayosisi ya Dodoma. Usharika wa Ebenezer ulianzishwa tarehe 21 Februari 2015 ukiwa ni mtaa chini ya Usharika wa Arusha Road...

Soma zaidi kuhusu sisi