Kuhusu sisi

Usharika wa Ebenezer ni miongoni mwa sharika 53 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ndani ya Dayosisi ya Dodoma. Vilevile, Usharika huu ni miongoni mwa sharika 27 za Jimbo la makao makuu ndani ya Dayosisi ya Dodoma. Usharika wa Ebenezer ulianzishwa tarehe 21 Februari 2015 ukiwa ni mtaa chini ya Usharika wa Arusha Road.

Usharika wa Ebenezer kipindi ukiwa Mtaa ulikuwa na takribani ya waumini 153, ambapo watu wazima walikuwa 58 na watoto 95. Wakati huo walikuwa wakisalia chini ya mti mmoja uliokua maeneo ya viwanja vya usharika kwa sasa.

Usharika wa Ebenezer ulifunguliwa rasmi tarehe 07 Aprili 2019 na Askofu Mstaafu wa kipindi hicho wa Dayosisi ya Dodoma Askofu Amoni Kinyunyu baada ya kuidhinishwa na vikao vya maamuzi vya Dayosisi ya Dodoma.

Usharika wa Ebenezer kwa sasa una takribani ya washarika 1,102 ikiwa 702 ni watu wazima na 400 ni Watoto. Vilevile, una Jumuiya 14 ambazo huendesha ibada za nyumba kwa nyumba.

Usharika unalea mitaa miwili ya Solowu na Mtungutu yenye takribani ya washarika 212, ambapo Mtaa wa Solowu una washarika 56, kati ya hao Watoto ni 25 na watu wazima 31. Mtaa wa Mtungutu una washarika 156, kati yao Watoto ni 45 na watu wazima 111.

Usharika wa Ebenezer unatekeleza maono ya Kanisa kwa kuwafanya watu wote wamjue Yesu Kristo na kuwa na uzima katika utimilifu wake kwa kuwapelekea Habari Njema za Neno la Mungu kutoka kwenye Biblia katika Upendo wa Kristo unaotolewa kwa watu wote.

Watumishi wa Usharika

  • Mch. .....

    Mchungaji kiongozi

  • Mch. ......

    Mchungaji Msaidizi

  • Ev. .......

    Mwinjilisti

  • Ms. ......

    Mhasibu

  • Mwl. .....

    Idara ya Muziki na Uimbaji

Saa za ofisi

Jedwali lifuata linaonyesha saa za kawaida za ofisi. Watumishi wote wanahudhuria ibada ya Jumapili na huduma husika siku hiyo.

MtumishiMondayTuesdayWednesdayThursdayFridaySaturdaySunday
Mchungaji Kiongozi9:00–16:009:00–16:009:00–12:009:00–12:00Ibada ya Jumapili
Mchungaji Msaidizi9:00–16:009:00–16:009:00–12:009:00–12:00Ibada ya Jumapili
Mwinjilisti9:00–16:009:00–16:009:00–16:009:00–16:00Ibada ya Jumapili
Mhasibu9:00–16:009:00–16:009:00–16:009:00–16:009:00–16:00Ibada ya Jumapili
Muziki na Uimbaji15:00–20:0015:00–20:0015:00–20:0015:00–20:0015:00–20:00Ibada ya Jumapili